Thursday

SMILING FACES WAMWAGA TUZO

TUZO INA RAHA YAKE
Mtangazaji wa kituo cha Luninga cha East Africa cha Jijini Dar es Salaam, Maimartha Jesse jana amepewa tuzo ya Mtangazaji Bora kwa kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2009 na kampuni ya mitindo ya Smilling Faces baada ya kufanya vyema katika taaluma hiyo na kupigiwa kura nyingi kupitia kampuni hiyo.

Mai alikabidhiwa tuzo hiyo mbele ya wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari, (Maelezo) hapa jijini. Ukiacha mtangazaji huyo mwingine aliyekabidhiwa tuzo na kampuni hiyo ni Martin Kadinda ambaye ametunukiwa tuzo ya mwanamitindo bora wa kiume mwenye vipaji zaidi
2008/2009.


NI MPANGO WA MUNGU KUWAONYESHA WATANZANIA KAMA UKIPAJI1 HIVYO NAMSHUKURU KILA MDAU ALIYETAMBUA NA KUTHAMINI KAZI ZA WANAMITINDO! HII SI KWANGU TUU BALI KWA WANAMITINDO WOTE NA KILA MTANZANIA MWENYE KIPAJI1 USISITE KUFANYA JAMBO JEMA KWA MANUFAA YA JAMII INAYOKUZUNGUKA, LEO NI MARTIN KADINDA KESHO UTAKUWA WEWE! GO FOR IT; MARTIN KADINDA

Maimartha akinadi tuzo yake! hongera sana

NI JAMBO JEMA KUMSHUKURU MUNGU PINDI AKUJALIAPO MAMBO MAZURI! SIKUTEGEMEA KAMA IPO SIKU WATU WATAGUNDUA NA KUTHAMINI KIPAJI CHANGU: MAIMARTHA JESSE


RICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS{RICHARD BUKOS}

Friday

His way to win a tittle!!



Henry Mwiki ni mwanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha(IFM)na yupo mwaka wa pili sasa! ana umli wa miaka 21, na ana mategemeo makubwa ya kufanya mapinduzi katika nchi ya tanzania! ni mapinduzi gani? mimi na wewe hatufahamu1 ila inabaki kuwa siri yake mpaka hapo atakapokuwa tayari kuwaeleza watanzania! hii ndio safari yake ya kuelekea ushindi!





Alionekana kupendeza zaidi na vazi la jioni! hivi ndivyo unavyoweza kutoka pindi ualikwapo katika hafla mbali mbalikuwa simple but smart, shati,suruali na kijikoti na muunganiko mzuri utakao kufanya uonekane vizuri mbele ya watu waliokuzunguka!



Hili ndio vazi lake la ubunifu kijana Henry! lilikuwa limechanganywa vitambaa mbali mbali na muonekano wake ulionekana kuwagusa wabunifu wa mavazi tanzania, kwani alitoka kitofauti
ASIA IDAROUS: Nguo yake nzuri sana, unajua uchanganyaji na uvaaje wake ni wakipekee! hayo ni maneno ya nguli wa mitindo tanzania.

Henry nadhani amejaliwa kipaji cha kuchagua nguo ambazo zinamfanya ang'ae zaidi pindi awapo juu ya stage na hii iliongeza misisimko katika show hii kwani kila mtu alijua kijana anaweza kutwaa taji hili la THE MOST HANDSOME MAN IN TZ, hapa a
kiwa ndani ya casual wear!!




Hatuwezi kujua majaji walitumia kigezo gani kutoa maamuzi ila mwisho wa yote kijana henry alishika nafsi ya pili! yaani the first runner up!na Khaleed kushika nafasi ya kwanza big up kijana, u did ur best and the rest was God's job. ila watnzania kauni tayari kwani kijana ameanza kuonesha makucha katika sanaa tanzania!!


tukutane wiki ijayo nitakapokueletea interview ya nguvu na washiriki wa shindano hili kujua maengi kuhusu wao na nini mategemeo yao baada ya kinyang'anyiro hiki!