Wednesday
Rangi Asilia ni kila kitu kwa mwanamke!!
Kila mwanamke amejaliwa rangi na mvuto kulingana na umbo na muonekano wake!! lakini baadhi ya wanawake wanashindwa kulijua hilo na kuanza kujichubua na kuleta muonekano na rangi zisizo zao!! na swala linalowapelekea kufanya hayo yote ni kulewa umaarufu na kutaka kujibadilisha wakidhani ndo watapendeza na kuvutia zaidi, kumbe wanajipotezea uzuri wao na kujipunguzia hata ile staha ya kuitwa mwanamke....
nasema haya yote kwa kuwa siku chache zilizopita nilikutana na Mtangazaji maarufu wa radio bibie Dina Marios na alinifurahisha kwa kuwa anaipenda sana rangi yake nyeusi na anajitahidi kwa kila khali kuitunza ili isije kuharibika na kupunguza mvuto katika ngozi yake..... je unadhani na wewe unapaswa kufanya hivyo?? uzuri si rangi nyeupe ila ni matunzo ya ngozi na jinsi gani unapangilia mavazi na muonekano wako mbele ya watu wanaokuona!!
la Muhimu, be comfortable with what your wearing na hakikisha unavaa nguo zinazoendana na wewe, oversize kwa mtu mwembamba si fashion na pia nguo za kubana kwa mtu mnene si fashion.. vaa nguo ambayo inaushika mwili wako kidogo ili isiwe bughuza kwako....
Baada ya kujua nguo zinazokufaa angalia accesories za kukufanya ung'ae zaidi, kwa mwanaume saa na bracelet zinasaidia kuongeza mvflani na kwa wanawake hereni na vicheni flani vidogo dogo vinakupa muonekano maradufu. . . usivae vae tu bora mradi unavaa, hakikisha unavutia ndugu yangu... dunia ya sasa hivi bila mvuto hauthaminiki....
Shukurani za dhati kwa model wangu Dina Marios!! maana ndo ameniwezesha nisidownload picha na nikatumia picha reall
Kaka ni kweli Dina ni mzuri sana kwa wajihi wake. Lakini lipo moja linaloshangaza na wadau tungependa atuweke wazi. Je nywele zake za asili ni zipi? kwa maana full time mwana dada huyu katinga ndani ya nywele za kununuwa. Hope she looks bomba zaidi akiwa natural zaidi kichwani
ReplyDeletewe mtu wa natural wewe.. acha tu!..
ReplyDeletebwana Dina amependeza na ukiangalia vizuri hilo alovaa ni wigi.. labda hataki kutia dawa nywele zake? lakini anataka aende na fashion, but inside ana "natural" hair..
anyways.. big up kaka, inatia moyo kuona kuna makaka ambao wanavalue a lady based on natural beauty and not plastic surgery!..lol