Thursday
GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 yapamba moto
Zoezi la kuwasaka wanamitindo wenye sifa za kipekee limekamilika jana katika hoteli ya giraffe ocean view baada ya wanamitindo kumi kupatikana katika mchujo wa awamu ya pili ambapo mchujo wa awali ulifanyika jumamosi iliyopita.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Unique Entertainment methuselah magese amesema kazi ya kuwasaka wanamitindo hao ilikuwa ngumu sana kiasi ambacho iliwachukua mpaka kusafiri kwenda mikoa ya jirani kama Tanga,Dodoma na pwani.
Giraffe unique model ni shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ambapo jula ya washiriki kumi watapanda jukwaani siku ya tarehe 24 desemba katika hoteli ya Giraffe hotel.
washiriki waliopita katika mchujo huo ni Dorah mhando,ritah samwel,bilkis suleiman,carina suleiman,asia dachi,calorine mwakasaka,diana mainason,mariam rabii,purity walele na jackline giyabe
No comments:
Post a Comment
sema tukusikie