Monday

Justin Timberlake akiri kuto kuongea na Britney kwa miaka 10 sasa

Msanii maarufu ndani ya Hollywood Justine Timberlake ambaye kwa kipindi cha miaka 5 sasa hajafyatua album mpya amesema yapata miaka kumi sasa hajazungumza na mpenzi wake wa zamani Britney spears, bila kutoa sababu ya msingi Justine alisema hivyo ndivyo mambo yalivyo kati yake na Britney Spears, nanukuu maneno yake anasema "Namtakia kila la heri katika maisha yake na mambo yake anayoyafanya japo hatujazungumza kwa miaka 9 au kumi sasa.. nakumbuka tulikuwa ndege wawili tuliokuwa tukipendana lakini sasa tunakuwa watu wazima na kila mtu anamaisha yake ya kuyajenga!! hatukuwa watu wa kawaida kipindi kile, tulikuwa watoto na tuliishi kwa kujenga ustaa"

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie