Wednesday

Victoria Beckham Agoma kuchukua likizo ya Uzazi

Mke wa Mchezaji mpira maarufu David Beckham, Victoria Beckham mwenye ujauzito wa miezi nane kwa sasa amegoma kuchukua likizo ya maandalizi ya mtoto wake anayetarajia kujifungua mwezi mmoja ujao Akijibu swali aliloulizwa kama anampango wa kupumzika akajibu,
"mapunziko ya uzazi??? ndo nini hicho? sina mpango wa kupumzika kwa sasa, nina kazi nyingi za kuandaa nguo mpya kama mnavyojua mimi ni mbunifu wa mavazi so napaswa kuwa makini na kazi yangu.. nitapumzika siku ambayo nitajifungua"

Victoria amekiri kuwa ni vigumu kuwa mama na wakati huo huo kuwa mwanamke mwenye mafanikio katika kazi unayoifanya, akaongezea kwa kusema ingawa Mumewe na watoto wake ni kitu cha kwanza katika maisha yake hayupo tayari na kuachana na kazi ya ubunifu na kuwa mama wa nyumbani kwasababu ubunifu wa mavazi ni kitu ambacho anakipenda na kinampa raha zaidi katika maisha yake

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie