Tuesday

Nick Minaj Awa Balozi wa MAC Cosmetics

Mwimbaji wa Rap Nick Minaj Inawezekana akawa anafata nyayo za Lady Gaga, Baada ya Hivi karibuni amesaini mkataba na Kampuni kubwa duniani ya Vipodozi ya MAC, Nick atakuwa balozi ya kampeni mpya ya bidhaa hizi inayojulikana kama VIVA GLAM 2012,

Kampeni ambayo itazinduliwa mwezi wa pili mwaka ujao, ambapo Nick atakuwa ndo msemaji wao na sura ya kampuni hiyo, Wakati huo huo Nick Minaj anatoa lipstick yake mwenyewe ambayo itakuwa ina rangi ya pink, nahisihii ni kutokana na dada huyu kuwa mpenzi wa rangi ya pink.

Kwa hivi sasa Nick minaj Yupo Miami akipiga picha za matangazo kwa ajili ya kampeni hii. kupitia ukurasa wake wa twitter Nick Minaj ameandika "hii shoot ni GAG, yaani siwezi kusubiri kuona jinsi watu wavyopendeza na hii Lipstick yangu mpya,kaeni tayari"

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie