Sunday

Rais wa Masharobaro on Set for his New Video (Bob Junior)

Video BY: Adam Juma From Visual Lab (Next Level)
Script of the Video written BY: Martin Kadinda
Wardrobe BY: Martin Kadinda and Styled by Noel Ndale
Hair Style & Make up Supervised BY: Martin Kadinda
Song Name: Nana nini
Produced at: Sharobaro Record
Artist: Bob junior
Kwa mara ya kwanza nimeamua kuandika Script kwa ajili ya Video hii, nadhani hii ni kutokana na msukumo nilionao katika kuboresha video zetu ili ziweze hata kuingia katika tuzo za Kimataifa,
Nimeandika Script ya movie ambayo itakuwa inaonekana ndani ya video hii, nimesimamia muonekano mzima wa bob Junioe kimavazi uonyoaji wa nywele, make up na mavazi ya wasichana wote walioonekana humu, ilikuwa ni kazi ngumu lakini naamini video ikitoka watanzania wenzangu mtapta cha kusema ili kama kunakosa likitokea lisijirudie tena, hii inaweza kuwa moja ya ajira yangu mpya nadhani.
Visual Lab ni moja wapo ya Studio maarufu hata Tanzania na kwakweli nimejisikia Vizuri sana kufanya kazi na Adam Juma, He is a very Understanding Person




Kosa lolote la kiuvaaji atakaloonekana nalo Bob Junior katika Hii Video msimlaumu yeye ila nilaumuni mimi maana ndio nilikuwa nikipangilia mavazi yake, alinieleza tu anataka kuwa Colourful so kwa jnsi nielewavyo mimi huo ndio muonekano alioutaka na katika zote nilizompangia hakuna hata moja aliyoikosoa.

Vipande vya movie itakayo kuwa inaonekana ndani ya Video hi sijviweka ili kukupa hamu ya kutaka kuona hapo baadae video itakapotoka ila jua imemshirikisha Actress mkubwa hapa Tanzania na Imefanyika nyumbani kwa Bob Junior, barabarani na ndani ya Vyombo vyetu vya usafiri (Daladala)...Video ni tamu balaa

1 comment:

  1. Anonymous02:00

    AYA MY DEAR TUNASUBIRI KWA HAMU HAYO MAMBO YAKO BILA SHAKA MZIGO UTAKUWA WA UKWELI.

    ReplyDelete

sema tukusikie