Saturday

HII IMENIUMIZA: LULU MICHAEL NI MDOGO WANGU

NIMEJUANA NA LULU YAPATA MIAKA MITANO TOKA TUKIWA SHULE WAKATI ANAANZA FORM ONE NA MIMI NIKIWA FORM 6 PALE PERFECT VISIO HIGH SCHOOL. KWA KIPINDI CHOTE LULU AMEKUWA MDOGO WANGU NA MTU WA KARIBU AMBAYE MARA NYINGI AMEKUWA AKINIHUSISHA KATIKA SWALA LAKE IKIWEPO UBUNIFU WA COVER YA MOVIE YAKE IITWAYO "FOOLISH AGE" HII NI KUTOKANA NA KUNIAMINI KWAKE NA MIMI PIA KUMWAMINI NA KUMWEKAA KARIBU YANGU NIKITAMBUA KUWA NI MSICHANA MDOGO MWENYE NDOTO NA MALENGO NA MAISHA YAKE...HILO LILINIFANYA NIMWONE NI ZAIDI YA RAFIKI KWANGU KWAKUWA NILIKUWA NAMLEA KATIKA MAZINGIRA YA KUMUONESHA NJIA ILIYO SAWA.. NASIKITIKA SIKU MOJA KABLA YA KUKUMBANA NA HILI BALAA ALILONALO ALIKUJA OFISINI KWANGU AKIHITAJI NIMSHAURI NINI AVAE KATIKA KILI MUSIC AWARDS.. ALINIAMBIA MARTIN NATAMANI SANA KUONEKANA TOFAUTI, NATAKA NISIVAE MAVAZI MAFUPI KAM AWALIVYONIZOEA WATU, MIAKA INAENDA NA NAPASWA KUJITAMBUA KAMA MIMI SASA NI DADA NA NINA WATU WANAONIANGALIA KAMA ROLE MODEL WAO. KUSEMA KWELI NILIFARIJIKA NIKITAMBUA LULU AMEKUWA NA AMEONA MBALI..... NINGEPENDA WATANZANIA WENZANGU NA WADAU WENZANGU WA BURUDANI KUTAMBUA LULU NI MSICHANA MCHESHI, MUWAZI NA MWENYE ROHO YA HURUMA, LULU HAJAJALIWA UCHOYO WA MAENDELEO..... MAGAZETI NA VYOMBO VYA HABARI VIMEANDIKA MAMBO MENGI KUHUSU LULU LAKINI MIMI NIMJUAVYO NI ASILIMIA 10 KATI YA 100 YANAWEZA KUWA NI KWELI.... HII NI VILE NIONAVYO MIMI, SIDHANI KAMA KUNA MTU NAWEZA KUBISHANA NA KILE NIKIONACHO MIMI KWAKUWA KILA BINADAMU ANAMTIZAMO WAKE NA HUO NDIO WANGU.

KILICHONIFANYA KUANDIKA HAYA YOTE NI HABARI AMBAYO IMEANDIKWA NA VYOMBO VINGI KUWA NIMESEMA LULU NI MJAMZITO WA MIEZI MITATU, HIVI KWELI MARTIN KADINDA KABADILIKA KUWA DAKTARI LEO HII WA KUWEZA KUJUA UJAMZITO UNAMIEZI MINGAPI? SIKU ZOTE NIMEKUWA NIKIMTANIA LULU KUWA ANATASHIKA MIMBA NA WATU HAWATAJUA KUTOKANA NA KUWA NA KITAMBI AMBACHO MWENYEWE ALISEMA NI CHA MAFUTA YA VINONO ANAVYOKULA, AKANIAMBIA HUWEZI UKAJUA LABDA NINAYO? HAYO NI MASIHARA AMBAYO MARA NYINGI TUMEKUWA TUKITANIANA KWAKUWA ALIKUWA ANAJUA NACHUKIA SANA MSICHANA MWENYE KITAMBI..  NAHESHIMU KAZI YA KILA MTU UNAWEZA KUKUTA KATIKA MAZUNGUMZO YANGU NA WATU WA KARIBU NIMEWAHI KUROPOKA JAMBO HILO AU SIJAWAHI PIA ILA KUTOKANA NA UKARIBU NILIONAO NA HUYU MTOTO HABARI IKAANDIKWA... SIWEZI KUTOA HABARI YA MTU BINAFSI TENA ISIYONIHUSU KWA MWANDISHI WA HABARI NA NINGEPENDA IWEKE WAZI KUWA NI MANENO YALIYOSIKIKA NDO HABARI IKAANDIKWA LAKINI SIO MARTIN KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI.... UKITAKA KUNIAMINI NIAMINI NA USIPOTAKA PIA SIKULAZIMISHI...

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie