Habari nilizozipata kupitia kwa mkurugenzi wa One touch zinasema,MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul,
anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya
watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa
hivi karibuni.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions,
Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo
katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.
“Jumamosi ijayo tutafanya
usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa
kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya
hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa
hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema |