Saturday

Inauma sana....

Ikiwa wewe muda wote upo juu ya kiti cha plastick unapika hapo katika ofisi unayofanyia kazi, au ni secretary wa ofisi flani una lalamika kazi yako ngumu na inachosha.. je huyu mtanzania mwenzako anayehangaika juani kutwa nzima na kuishia kupata elfu moja au mia tano kwa siku yeye asemaje?
binadamu mwisho wetu ni pale tunapokumbwa na mauti na kuelekea kusiko julikana.. je unamuomba mungu kifo chako kiwe salama? ufe bila mateso?tazama binadamu tulivyo wanyama, mwizi kakuibia simu au elfu tano katika pochi yako unamtoa uhai wake kama vile wewe ndiye uliyemuumba..hivi kweli na wewe unatamani kufa kifo hiki? vyombo vya dola vimewekwa kwa ajili gani? unajua sababu iliyompelekea kuiba? tusikurupuke na kushiriki mauwaji ya wenzetu kwa Mungu tunatoa maelezo gani ya kujitosheleza kwa haya tunayoyatenda?

Unakitanda kizuri chenye godoro zuri la kuvutia unashindwa tu kutoa shuka na kulifua mpaka Dada wa kazi hapo nyumbani kwako au kwenu akufulie.. tazama vijana hawa wasiojua watakula nini kwa siku hiyo au kulala wapi kwa usiku unaokuja wanahangaika katika vituo vya daladala japo wapate muda wa kupumzika...

4 comments:

  1. Anonymous02:43

    si bora huyo ambae anahangaika kubeba mzigo apate mia tano kuliko huyo anaeiba kipigo ni halali yake.

    ReplyDelete
  2. Anonymous04:15

    Mdogo wangu nakufahamu tu kwa kuona sura yako kwenye blog yako lakini kwa maneno ulosema hapo kwa huyo kijana aliyeuawa naamini una hofu ya Mungu. Mungu akubarikia sana. tuiombee Tanzania yetu.

    ReplyDelete
  3. Anonymous03:27

    KweliINAUAMA.fikiria wewe ni mzazi, kijana wako wa kiume mdogo kwa umri na anonekana unanguvu na afya ya kutafta elimu ili ije imusaidie "for his future".kutwa nzima anawaza jinsi ya kujipodoa ili siku iyo azunguka kwenye vi birth day alivyoalikwa au wanavyotaka kuzamia na kundi wanawake analoongozana nao kila kukicha kama vile hayo ndio yatakua maisha yake mpaka uatkapozeeka...kama mzazi inauma sana...Dogo Badilika kama kijana mwenzio naona unapotea maisha unayoanagaika nayo hayotokusaidia lolote na utakuja kukumbuka umri ushaenda...sikiliza nyimbo ya UMRI. TMK WANAUME.kama kawaida yenu wenye maisha ya "kufake" mkiambiwa ukweli huwa mnadai Haters ila ujumbe umekufikia.

    ReplyDelete
  4. Anonymous 3... thank you very much for your comment and may God always bless with the God heart you have.. i think ur a very wrong na akili zako zimetawaliwa na ulimbukeni na chuki binafsi juu ya maisha ya watu flani flani.. au maybe hii comment yako umekosea pa kuweka maybe sio kwa ajili ya blog hii.. Katika kumbukumbu nilizonazo za maisha yangu mimi si mpenzi wa kuhudhuria shughuli za watu za kwao binafsi hata katika hizo birthday unazosema sihudhuliagi sana sana za ndugu zangu so maybe huyo unayemuongelea ni someone Else.. if you don know am proffesional manager niliyesomea Evin school of management ambayo ni tawi la London institute of management coz maalumu ya management i was specifical based on event management sasa unaponiona katika event huwa sijaenda kuuza sura bali nakuwa kazini.. fanya utafiti kabla hujaandika comment zako maana sometimes unakuwa umepoteza muda kuandika upuuzi!!

    ReplyDelete

sema tukusikie