Thursday

Kutoa ni Moyo na wala Sio utajiri Ulionao....

Mpangilio wa picha sio mzuri sana lakini naamini ukisoma maelezo tutaelewana na tutakwenda sawa.. kupitia ukurasa wangu wa Facebook wakati wa kwaresma niliomba watu mbali mbali tuungane pamoja katika kwenda kutembelea kituo cha watoto yatim ana baada ya hapo sikuliongelea tena swala hilo.. ile safari ilifanikiwa kwa msaada mkubwa wa dada yangu kipenzi Margareth ambaye ndio alikuwa msimamizi wa kila kitu akisaidiana na watu wengi cant mention all of you but katika picha wanaonekana.. tar 9 april tukafunga safari mpaka mbagala zakhem ambapo kuna kituo kinaitwa Kwetu mbagala Home.... ni kituo kinachotunza watoto wa kike tu kuanzia mwaka mmoja mpaka 15..

Tulijitahidi kupata chochote ili tuweze kula lunch na watoto hawa na kweli iliwezekana...si mbaya mtoto akipata chakula na tunda bila kusahau kinywaji....

Dada mwenye blouse ya pink ndio alikuwa mwenyeji wetu kwa siku hiyo maana wahusika walikuwa wametoka kwenda kufanya shughuli nyinginezo za kuimarisha maisha ya watoto hawa kwa kipindi chote watakachokuwa kituoni..
Wenye magari walijitokeza kwa wingi kuhakikisha tunafika salama na kwa haraka kuliko tungetumia public transport.. asanteni sana...






Mlo wa mchana kwa pamoja


Mr&Mrs watarajiwa wakipata mlo na bro Faraji kwa nyuma akidoea picha.

ubovu wa maeneo ya michezo...

Tusiangali mazuri tu waliyonayo watoto hawa.. kubwa ambalo nimeliona hapa ni uchakavu wa maeneo ya michezo na moja ya bembea unaiona hapo ikiwa imelala pembeni kwa kuvunjika.. natamani ningepata mfadhili akanisaidia kuimarisha maeneo haya ya michezo kwa watoto hawa maana naamini michezo ni sehemu ya makuzi ya watoto hawa.. plz aliye na chochote tusaidiane katika hili..

Moja ya swala wanalopewa mkazo zaidi watoto hawa ni kuwa wasafi kuanzia mazingira ya wanapolala mpaka wao binafsi..

ki ukweli watoto hawa ni wasafi na wanafuata maagizo wanayopewa na walezi wao.


Wana umeme wa solar endapo umeme wa tanesco ukikatika....

group picture1

group picture mimi nikiwa cameraman wao....

group picture ilikamilika.

Kweli binadamu ni mtoto hata akiwa na ndevu nyeupe.. watu wazima na akili zetu baada ya kuona bembea tukaiparamia kwa pupa...wenye kilo chache tulikuwa tunawarusha juu kama upepo..

Kimmly dada yangu alivamia shamba la watu kwa mbwe mbwe kama anajua kuchuma mboga kumbe hana lolote...

Kiongozi wa safari yetu dada Margareth alipata nafasi ya kusema machache kwa niaba ya watu wote alioongozana nao...

Vile vidogo tulivyokuja navyo ndivyo tulivyowaomba watoto wetu wapokee..


Elimu ndio zawadi pekee ambayo mtoto anaweza kupewa na wazazi wake au walezi wako na ikadumu kwa maisha yake yote.. hivyo tulidhani vifaa vya elimu ni bora zaidi kwa watoto hawa..

Kidogo hichi hichi tulichonacho tugawane na wale wasionacho

Mwisho wa kazi hii tuliyotumwa na jamii yetu nilijipatia mchumba... anaitwa Predigander... she is a very nice girl... anajua nini thamani yake kama mwanamke si mnaona kajifunika nywele hapo?



Hii sio safari yetu ya mwisho nitajitahidi mimi na wale wenye moyo wa kuboresha maisha ya wenzio wasiojiweza kwa pamoja kuhakikisha tunasaidiana kwa kile kidogo mwenyezi Mungu alichotujalia maana leo ni kwao na kesho yaweza kuwa kwangu au kwao... ya Mungu mengi..Amen

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie