Tuesday

Flaviana Matata Azindua "FLAVIANA MATATA FOUNDATION"

Ikiwa ni siku chache tangu mafanikio ya binti mdogo wa kitanzania Flaviana matata kuonekana kutokana na kazi anayoifanya hivi sasa ya uanamitindo huko nchini marekani, Binti huyu ameamua kuzindua Foundation ambayo itakuwa ikijihusisha na uwezeshaji wa wanawake na watoto wasioweza kupata huduma mbali mbali za muhimu katika maisha yao.. Akizungumza wakati wa Uzinduzi huu Flaviana Matata amesema "Elimu ni jambo la muhimu kwa kila binadamu na linahitaji Fedha ili kuhakikisha linapatikana kwa wakati muafaka, hivyo nitajitahidi kupitia Flaviana Matata Foundation kuwawezesha wanawake na watoto kupata elimu bora!!
Mwanvita Makamba ambaye ni mmoja wa walezi wa Foundation hii akitoa neno la ufunguzi wakati wa uzinduzi wa Foundation hii uliofanyika ndani ya Hotel ya Kempisky!!
Wadau mbali mbali waliohudhuria uzinduzi huu kutoka kushoto Teddy mapunda, Babla Hassan And Salama jabir

More pictures za fashion na nyinginezo kutoka katika shughuli hii zinakuja.. hizi ni kwa msaada wa fullshangwe blog

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie