Monday

DARASA: Epuka Msongo wa Mawazo (Stress)

Mara nyingi tumekuwa tukikumbwa na msongo wa mawazo kutokana na shughuli zetu za kila siku katika maisha, Endapo wewe ni mdau wa burudani kwa upande wowote, labda ni mwanamziki, mtangazaji, muigizaji,mwanamitindo au hata mshereheshaji katika hizi kazi zetu tunakutana na watu wengi kila siku na wanakuwa na hamu ya kukujua kutokana na kazi unayoifanya au nia mbali mbali wanazozijua wao wenyewe, Sasa kitendo cha kuwa na watu wengi karibu inamaanisha na mahitaji kutoka kwako yanaongezeke, trust me kama unafamilia ambayo inakuangalia, wasanii wenzako wanakuangalia na wapenzi wa kazi yako nao wanakuangalia Lazima utakumbana na msongo wa mawazo, maana utakumbwa na bili za kuzilipia, watu wa kuwasaidia kiushauri na hata kimahitaji au kushiriki shughuli mbalimbali ukiachilia mbali kazi yako binafsi.. Je ni jinsi gani unaweza kuepuka msongo wa mawazo kutokana na hayo yote?




1.Tambua chanzo cha msongo wa mawazo ulionao, je ni kazi yako na eneo lako la kazi?? je ni maisha yako binafsi (Lifestyle), rafiki au ndugu zako au wapenzi wa kazi zako??

2. Tambua huwa unakuwa katika hali gani pindi unapokuwa na msongo wa mawazo.

3. Mara nyingi kitu gani huwa kinakusaidia kupunguza huo msongo wa mawazo awali


Jinsi ya kuepukana na Stress

Kuna baadhi ya Stress ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya kutatua shinikizo la msongo wa mawazo


1. Jifunze kusema "hapana" hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako... sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.


2.Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, unajua ukikaa chini na kufikiria utagundua kuna mtu flani au kundi flani la watu ndo linalokuleta msongo wa mawazo, sasa kaa nao mbali kabisa.


3. Simamia mazingira yanayokuzunguka

mazingira yanakuzunguka yanaweza kuwa sababu ya stress zinazokukumba, mazingira yapo nayozungumzia mimi hapa? njia unayotumia kwenda kazini au kurudi nyumbani ina foleni sana? hiyo nayo inawea kuwa sababu ya stress ulizonazo, lakufanya epuka matumizi ya barabara kwa wakati huo, mazingira ya soko wakati wakufanya manunuzi ya bidhaa mbali mbali yanakupa stress? nenda katika supermarket maana kwa kiasi flani kuna utulivu na hali ya hewa nzuri


4.Epuka Hasira za haraka, kuna ya mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka nao ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi


5.Tengeneza orodha ya vitu anavyotaka kufanya sikuhiyo asubuhi tu ukiamka, mara nyingi unapaswa kujua mambo ambayo ni ya lazima kuyafanya kwa siku ambayo unaianza ili ikifika jioni usiwe na viporo, katika orodha yako tenganisha orodha hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa mawazo.


Naomba niishiw hapa kwa leo maana nimewaonjesha yale ninayoyajua na ambayo nimejifunza, swala la kuondoa msongo wa mawazi linapaswa kuangaliwa kiundani zaidi maana ni pana sana, hapa juu nimeongelea kuepuka stress ambazo si za muhimu ila kuna swala la saikolojia ambalo sijaligusa kwakuwa mimi si mtaalam wa saikolojia. siku nikijua mengi zaidi kuhusu stress nitatoa darasa zaidi.


4 comments:

  1. Anonymous07:09

    thanks for this kaka
    jimmy james k

    ReplyDelete
  2. Anonymous00:04

    asante sana anko

    ReplyDelete
  3. Anonymous08:16

    Umesema sana lakini unajua akili ndio wazo, mtu unapokuwa na akili ndio unaweza kutoa wazo kwa maana hiyo basi utakuta mtu anajimilikisha mambo mengi kwakuona atamudu matokeo yanapokuja ndio wazo linakuja kuwa simudu hali yakuwa ameshajimilikisha mambo kupita uwezo wake na hapo basi ndipo panatokea msongo wa mawazo ambao umesababishwa na akili, kwahiyo akili nyingi huondoa maarifa.

    ReplyDelete

sema tukusikie