Monday

Ndoa ya Jlo na Marc Anthony Yaanguka

Ikiwa ni Mwezi mmoja tangu kusherekea miaka saba ya ndoa yao Jaji wa American Idol Jennifer Lopez na mumewe Marc Anthony walimeamua kutalikiana,



Wanandoa hawa waliofunga ndoa mwaka 2004 mwezi wa Sita, walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha miaka mitatu iliyopita wamesema maamuzi waliyoyafanya ni magumu lakini imebidi yafanyike ili kila mmoja aweze kuendelea na maisha yake binafsi
Katika nakala yao walioitoa kwa vyombo vya habari wanasema
"tumeamua kuvunja ndoa yetu,ingawa ilikuwa ni jambo zito na gumu, hii ni kutoka na kufikia hitimisho ya mambo yaliyokuwa yametawala mahusiano yetu, ni wakati mgumu sana kwetu na tunashukuru kama mkiheshimu uhuru wa mambo yetu binafsi"


Jinsi nilijuavyo mimi hii ni ndoa ya tatu kwa mwana mama Jennifer Lopez, moja ilivunjika mwaka 1998 na ya pili ilikuwa ya yule dancer ambayo ilianguka nayo mwaka 2004, ambapo kwa Marc Anthony hii ni ndoa yake ya pili baada ya kwanza kuvunjika mwaka 2004 pia.
Najiuliza Jlo may atarudi kwa Diddy maana she is now single au atamove on to a new man?

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie