Thursday

Muonekano wako Uwapo Ufukweni



Ufukweni au beach kama wengi mlivyozoea mara nyingi ni eneo ambalo huwa tunaenda kupunga upepo na kutuliza akili zetu kutokana na yale tuliyopitia kwa kipindi kilichopita! familia nyingi au vijana wengi kama nijuavyo mimi hupenda kwenda ufukweni wakati wa weekend hii ni kutokana na kuwa ndio wakati pekee tunapata nasi.Tukumbushane mambo ya muhimu uendapo ufukweni ili usiwe tofauti na wenzio utakaokutana nao huko, kwa vijana wakiume hizi ndizo kaptula zinazotufaa kwakuwa hazibaki na maji mwili wala kushika maungo yetu maana kuna watu huwa hawana amani kuogelea na nguo zao za ndani kwakuwa huwa wanahisi wanajichora maungo yao, hivyo basi ukipata kaptula kama hizi mambo yako yatakuwa salama kabisa.

Kitu cha muhimu kuzingatia wakati wa kununua kaptula ya kuogelea, chagua rangi zinazoendana na rangi yako ya ngozi, mtu mweusi hauendani na rangi kali, kama orange, njano mkozo au kijani kikali... tafuta kaptula za rangi iliyopoa.Ndugu zangu kutokana na mchanga wa Beach hatuendi na Raba ila sandals au kwakiswahili fasaha viatu vya wazi, jitahidi kupata sandals nyepesi zisizo nzito ili uweze kutembea kwa wepesi katika ule mchanga wa baharini

Zingatia rangi ya Sandals inayoendana na kaptula utayaokuwa umevaa ili ung'ae na kuvutia, who knows? inaweza kuwa your luck day kama uko single ukamvutia binti ambaye anaweza kuwa yupo ufukweni kwa siku hiyo

mara nyingi kuna vumbi jepesi ambalo huwa linatimka kutokana na upepo wa baharini, jitahidi kuwa na sun glasses kwa ajili ya kuzuia vumbi hilo kuja moja kwa moja machoni kwako, huwa kunakuwa na jua kali wakati mwingine hivyo miwani hiyo hiyo itakusaidia kuepukana na miale mikali ya jua.Miwani ipo ya rangi tofauti, chagua inayokufaa

Mwisho kabisa unahitaji lotion za jua kwa ajili ya ngozi yako, jua huwa linakuwa kali sana na linaweza kuharibu ngozi yako usipokuwa makini, hivyo ningependa kukushauri kuwa na sun lotion ambayo inaendana na ngozi yako.


Kabla ya kutumia lotion hizi jitahidi kumuona mtaalamu wa ngozi ili uweze kupata lotion inayoendana na ngozi yako maana lotion nyingi za jua zimetengenezwa kwa ngozi za watu weupe (wazungu)

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie