Wednesday

Angeline Jolie Anachukia "Kukumbatiana"

1. Angelina Jolie anatatuu ya herufi H ambayo imechorwa kwa upande wa ndani wa mkono wake wa kushoto, Tatuu hiyo inamaanisha jina la kaka yake aitwaye James Haven Voight ambaye ni mtu wake wa karibu sana.

2.Mwaka 2000 Angeline jolie na kaka yake walizungumzia tetesi za kuwepo kwa uhusiano kati ya wawili hao kutokana na kitendo chao cha kuonekana mara nyingi wakipigana mabusu ya mahaba hadharani kitendo kilichoanzisha hisia kwa watu kuwa wanaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi,Siku chache zilizofuatia James alisema anamchukulia dada yake kama mwanamke kamili, anasema hajaona mwanamke mwenye kuweza kumzidi dada yake huyo mpenzi.

3.Alipokuwa mdogo Angeline jolie alitamani sana kuwa Vampire na alikuwa kashaanza kukusanya vitabu vinavyohusu maisha ya Vampire. Baadae aligundua kuwa ndoto zake ilikuwa ni kuwa muongozaji Mazishi. .

4. Angelina Jolie pia amewahi kusema kuwa Muigizaji wa kike Gena Rowland ndio alimfanya ajiingize katika uigizaji. na Kwa bahati nzuri angeline julie amewahi kushiriki filamu moja na Star huyo katika filamu ya Playing By heart (1998) na Taking Lives (2004)

5. Mama mzazi wa Angelina Jolie bi.Vivienne Bertrand alimchagulia jina yule mtoto wake wa tatu aliyemuasiri kutoka Vietnam, mtoto huyo alipewa jina la Pax

6. Angelina Jolie alijiingiza katika uanamitindo akiwa na miaka 14 na alipotimiza miaka 18 akaachana na modeling na kuingia katika uigizaji.

7. Angelina Jolie’s alionekana kwa mara ya kwanza katika maigizo mwaka 1982 alipokuwa na miaka 7 alipoonekana katika filamu ya baba yake iliyofahamika kwa jina la Lookin' to Get out.

8. Akiwa mtoto, Angelina Jolie alikuwa na nyoka wawili aliyowaita Vladimir na Harry Dean Stanton. Kuweza kucheza na Nyoka toka akiwa mdogo kulimwezesha kuweza kucheza vizuri katika filamu ya ALEXANDER

9. Jolie ni shabiki mkubwa wa Liverpool Football Club hii ni kutokana na mwanae Maddox kutaka kuchezea timu hiyo

10. Angelina Jolie Hana mwandishi wa habari au mzungumzaji wake, anafanya kila kitu yeye mwenyewe bila msaada wa afisa mahusiano.

Na kubwa kuliko zote Angeline jolie anachukia sana swala la kukumbatiana. anasema hapendi kabisa kukumbatiana na mtu yoyote.


No comments:

Post a Comment

sema tukusikie