Monday

Dina Marios umenigusa na hii Post on Your Blog

Hii P0st nimeona katika Blog ya Mtangazaji wa CloudsFm na nikaguswa nayo kwasababu asilimia kubwa ya bloggers wanakutana na aliyokutana nayo yeye hivyo nimeona niibebe kama ilivyo na kuipost hapa pia! ujumbe uwafikie wote unaowahusu.

Mara kadhaa wadau wengi huniuliza ninawezaje kuvumilia maoni ya watu wachache wenye matusi na kejeli juu yangu!?


KAULI YANGU


1.Kama binadamu wakati mwingine huwa naumia ila ninajua kwa nini watu kama hao wapo,wapo kwa sababu mimi ni Dina Marios.


2.Bila wao kujua hawa watu wananikubali sana ila wanachukia kwa nini wananikubali.


3.Watu hao wana hasira na maisha yao,wao wenye binafsi lakini kwa sababu hawajui namna na kukabiliana na hasira zao huzimalizia kwangu kwa sababu anaona kuna jambo fulani nimefanikiwa kumzidi.


4.Kwenye comment nzuri 50 inapotokea comment 1 ya matusi na kejeli ina maanisha nini?inamaanisha wanaoniombea mema ni wengi.


5.Kwa sababu najua tatizo la mtu huyo ndio maana huwa ninaweka comment yake.Akiiona yeye anafarijika na nafsi yake kuwa ameniweza hiyo ni relief ya ugonjwa unao msumbua coz nilikuwa nauwezo wa kuifuta.


MFANO
hujafanya chochote cha maana hamna asiyejua kupika sausage na mayai kwanza embu uwe una update blo yako na vitu vya maana sio uwo usenge acha uvivu msenge wewe... mnene kama pipa
Definition ya mtu mwenye maoni kama haya kwanza ana msongo wa mawazo,ana matatizo yake mwenyewe ila kwa sababu hawezi kudeal nayo anatafuta wapi pa kutolea hasira zake.Kwa nini si mtu mwingine ni mimi?ni kwa sababu nini ni threat kwake.Kama angekuwa better than mimi bila shaka asingekuwa hata na muda wa kutoa comment za matusi.
Pia hajiamini hivyo anatafuta mtu wa kumshusha ili aweze kulingana na yeye kihisia.Kama angekuwa anajiamini sana basi angeweka jina lake tumjue.
Maoni ya ku-critisize yanaruhusiwa ila yanapokuwa ya matusi tena yasiyo na sababu inaonyesha mtu huyu ana ugonjwa wa akili.
Unaponiita mnene kama pipa,tinginya sijui vitu gani kwani nina kilo 100,200,300!!!una uhakika huko kwenu hakuna watu wanene??ndugu zako jamaa zako??

Pls wale wenye comment za hivi waoneni phsycologist mapema kwa ajili ya councelling kabla hamjapata matatizo.Its not healthy at all au ongea wadau wakusaidie kimawazo.
Mwisho namaliza kwa kusema nahitaji sana challenge/changamoto kutoka kwako na sio matusi.

2 comments:

  1. Anonymous07:47

    what is your twitter account name

    ReplyDelete
  2. Martinsurvivor its my username on twitter

    ReplyDelete

sema tukusikie