Tuesday

Beyonce Aanza kukinadi kitumbo chake

Ikiwa ni siku chache toka mwanadada Beyonce atangazie dunia kuwa anaujauzito wa rapper Jay Z ambaye ni mume wake, Beyonce ameonekana akijiachia vilivyo katika pwani ya Croatia Ambapo yuko huko katika mapumziko akiwa na mumewe na mdogo wake Solange.... Wataalam wa mambo wanasema mwanadada huyu ameamua kuvaa kivazi kinachoonesha eneo kubwa la tumbo lake ili watu ambao hawakuamini kama kashika mimba waweze kuishuhudia kwa macho yao wenyewe.
Katika interview alizowahi kuzifanya beyonce nakumbuka alisema ni lazima ashike mimba kabla hajatimiza miaka 30 na hili kweli limetimia kwakuwa jumapili hii Beyonce atakuwa anatimiza miaka 30. napenda kumtakia kila la heri katika malezi ya mimba yake mpaka hapo atakapojifungua!! zile perfomance zake ambazo huwa anazifanya akiwa na viatu virefu ataendelea nazo????

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie