Tuesday

NAWACHUKIA WAMILIKI WA SALOON HASA ZA KIUME.

SINA NIA MBAYA KWA KUANDIKA KICHWA CHA HABARI NILICHOANDIKA ILA NIMEKUWA NIKIKASIRISHWA SNA NA HUDUMA NINAZOZIPATA PINDI NIENDAPO KATIKA SALOON MBALI MBALI, HII HAIJANITOKEAPEKE YANGU LAKINI KWAKUWA NINA NAFASI AMBAYO INANIWEZESHA KUONGEA NA KUSIKIKA NA WATU WENGI. NAWEZA KUANZA KWA KUSIFIA KWA MAPOKEZI MAZURI TUNAYOPATA TUKIFIKA... HILO MNAHITAJI PONGEZI.


KIMBEMBE KINAANZA PALE NINAPOHITAJI KUNYOLEWA.... MARA NYINGI SINA TATIZO HAPA NAPO JAPO NIKIHAMA SALOON NA KWENDA KWENYE SALOON NYINGINE MARA NYINGI VINYOZI HUWA HAWANA UBUNIFU WA KUMNYOA MTU KULINGANA NA KICHWA CHAKE.... WANANYOA BORA MRADI WAMALIZE KAZI NA UWALIPE.. SASA NAJIULIZA NYINYI WAMILIKIWA HIZI SALOON HUWA MNANYOA HAPA HAPA? MANAZIONA KASORO TUNAZOZIONA WATEJA WENU? KWANINI MSITAFUTE VIJANA WENYE UBUNIFU NA UWEZO WA KUNYOA VIZURI? MAANA MIMI NIKINYOLEWA VIBAYA.. WIKI YANGU YOTE HUWA INAKUWA MBAYA.

BAADA YA KUNYOLEWA KUNA HUDUMA MBALI MBALI HUWA ZINATOLEWA KAMA FACIAL STEAMER NA SCRUB... WALE WASICHANA WANAOTOA HUDUMA HII NDO HUWA WANANICHEFUA ZAIDI, SIJUI NDIO WAMEKARIRISHWA KILA MTU ANAHITAJI SCRUB.. MBAYA ZAIDI HAWAJUI KUANGALIA NGOZI YA MTU... SCRUB MOJA WALIONAYO NDIO HIYO WATEJA HATA 40 MTATUMIA.. HAWAJALI KAMA NGOZI YAKO NI KAVU AMA YA MAFUTA... WANAKUPAKA... JITAHIDI KUWA NA WATAALAMU WA NGOZI AMBAO WATAKUWA WANAWASHAURI WASICHANA AINA YA SCRUB YA KUMPAKA MTU.. MKIWA NA MSHAURI  WA NGOZI NI RAHISI KUHAKIKISHA NGOZI ZA WATEJA WENU HAZIHARIBIKI KWA UBOVU WA HUDUMA ZENU...WASICHANA MLIKUWA NAO KATIKA HIZI SALOON ZENU HATA COURSE YA SALOON HAWAJAWAHI KUSOMA IWEJE LEO AHANGAIKE NA NGOZI YANGU?? MNANIKERA SANA NDUGU ZANGU. NA OLE WENU NIJE TENA MNIPAKE HIYO APRICOT YENU.


BAADA YA MTITI HUWA MARA NYINGI HUWA WANAKUWA NA VITAMBAA FLANI AMBAVYO WANATUFUTIA USONI.....HICHO KITAMBAA KIMEFUTIA WATU WANGAPI TOKA ASUBUHI? YAANI NIKIINGIA SALOON MWILI HUWA UNANISISIMKA MAANA HUWA NAHISI KUCHANGANYIKIWA.


4 comments:

  1. True dat Martin. Hygine ktk salon ni ndogo sana na wamiliki hawaajiri proffessioanals. Wanashindwa kutambua kuwa huduma bora ni kigezo cha kuimarisha biashara. Ni mengi sana yanaonekana kuwa ni mapungufu na hii ni opportunitity kwa wageni. Hata salon watafungua Wakenya na wazungu hapa nchini kwetu.. Ni hayo tu

    ReplyDelete
  2. Anonymous12:36

    this may sound harsh anyways it's the truth..
    mambo ya saluni hasa kwa kina kaka bongo bado.I think you are looking for a five star treatment in cheap place(subiri utaipata)..for now you cud try serena(u might get that kind of treatment)lol..everyone is trying to survive,like u do,i blv u dont have the knowledge in textiles/garmets whatsoever(u r not even planning to learn) ila unabangaiza..u dont like the services dont go..i dont dig your single button i dont wear,SIMPLE..no hard feelings bro

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous00:15

      hahahaaaa me like you alot��

      Delete
  3. Mercy23:30

    Pole sana bro,hizo kash kash zipo hata huku kwe saluni za kike tunaoshewa shampoo yoyote tu bila kujali aina ya nywele,mafuta utapakwa yoyote bila kuulizwa.taulo bichi unafutiwa na wewe na vitana ndo balaa kina nywele ya mtu mwingine nawe watwisha hikohiko in short ni kichefchef tu

    ReplyDelete

sema tukusikie