SAMAHANI SANA KWA KUANZA NA UTAMBULISHO WA PICHA LAKINI NADHANI PICHA ZINAELEZA MENGI ZAIDI KULIKO MANENO YANGU... JINA LANGU NAITWA MARTIN KADINDA AMBAPO NAJIENDELEZA KIMAISHA NA KUWASAIDIA WALE WANAOHITAJI MSAADA WANGU KWA KUPITIA KAZI ZA SANAA, NIMEJIAJIRI MWENYEWE KWA KUPITIA KIPAJI CHANGU CHA UBUNIFU WA MAVAZI NA SHUGHULI NYINGINE MBALI MBALI ZINAHUSISHA UBUNIFU... SABABU KUBWA YA KUANDIKA BARUA HII NI KUTOKANA MACHUNGU NILIYONAYO KWA NCHI YANGU NA WATU WAKE... ANGALIA PICHA YA HAPO JUU.. HIYO NI TIMU YA MICHEZO YA MAREKANI INAYOSHIRIKI KATIKA OLIMPIC AMBAPO WAMEVALISHWA NA MBUNIFU WA MAVAZI ... ANGALIA JINSI NGUO ZINAVYOPENDEZA... HII KWAO NI NJIA YA KUTANGAZA UWEZO WAO SIO TU KATIKA MICHEZO BALI KATIKA MAVAZI.. HII NI KUTANGAZA SOKO LA WABUNIFU KUPITIA KAZI ZAO.... USHIRIKIANO ULIOPO BAINA YA WANAMICHEZO NA WABUNIFU NI MKUBWA NA WENYE KULETA MASILAHI KWA PANDE ZOTE MBILI.... SIDHANI KAMA KUNA MTU ANAKUMBUKA KAMA KATIKA MAVAZI YALIYOVALIWA NA WANAMICHEZO WETU KATIKA OLIMPIC KAMA YALIKUWA NA UTAIFA ZAIDIBENDELA WALIZOZISHIKA.. ZILE SUTI WALIZOVAA ZIMEBUNIWA NA NANI KAMA SIO ZIMENUNULIWA? ZILE TRACK SUITS JE? NAZO ZIMENUNULIWA.. KWELI MTU KAMA SALIM ALI WA MTOKO DESIGNS ASINGEWEZA KUTENGEZA HIZO NGUO? BASI HATA KALI ELEGANCE KAMA SIO MARTIN KADINDA WANGEWEZA KUTENGENEZA HIZO SARE TENA BURE ILI KUWEZA KUTANGAZA KAZI ZAO KATIKA SOKO LA KIMATAIFA... TUMEKUWA TUNASHINDWA KATIKA MASHINDANO MENGI KWASABABU TUMEKAZANA NA VITU VYA NJE NA KUSAHAU VYA KWETU.. WASHIRIKI WA MASHINDANO MENGI YA KIMATAIFA WANAKURUPUSHWA NA KUPELEKWA HUKO BILA MAANDALIZI YA KUTOSHA NA NDIO MAANA KIAL SIKU TUNAKUWA WA MWISHO... NI AIBU AMBAYO TUNAITAFUTA WENYEWE ALWAYS. JUZI JUZI TU HAPA TUMESHUHUDIA NGUO ZA ATC ZIKIPIGIWA KELE KUWA ZIMETENGENEZWA KWA GHARAMA KUBWA NJE YA NCHI NA NI UTUMBO MTUPU.. SASA KOSA NI LA NANI? NAHISI NI SERKALI KWAKUWA HAKUNA NAFASI WANAYOPEWA WABUNIFU KATIKA KAZI MUHIMU KAMA HIZO.. MADUKA MAKUBWA YAMEKAZANA KULETA NGUO KUTOKA NJE YA NCHI NA KUSHINDWA HATA KUWEKA LINE MOJA YA NGUO ZA WABUNIFU WA TANZANIA KATIKA MADUKA YAO.. INGEPITISHWA SHERI AMBAYO INAWALAZIMA WAINGIZAJI WA MAVAZI WAKUBWA KUWA NA ASILIA KUMI YA MAVAZI YALIYOBUNIWA NA WABUNIFU WA KITANZANIA.. HIYO ITASAIDIA KUBORESHA KAZI ZA WABUNIFU WETU |
|
sawasawa kaka unacho zungumzia ni ukweli mtupu,tena hongera na ongeza bidi katika kujenga taifa letu kwa upande wako kwani ndo maendeleo yanapatikana hivyo.
ReplyDelete