Wednesday

Naililia Japan na Dunia kwa ujumla!!

Ikiwa boti zilivuka bahari na kutupwa nchi kavu unadhani kuna watoto watakuwa walisalimika hapa? hili ni pigo kubwa kwa dunia na zaidi kwa japan.. nawalilia watoto wadogo walifariki katika janga hili.. wapo waliokuwa na mategemeo na ndoto kubwa katika maisha yao na taifa leo!!
Nchi yenye maendeleo na udongo wa rutuba imebadilika kuwa janga.. ni harufu ya vifo na umaski ndio umetawala kwa sasa!!
badala ya kusafisha jiji kwa takataka za vyakula au bidhaa flani... leo wanakusanya miili ya waliofariki kwa janga hili la Tsunami
Yako wapi yale maghorofa mazuri yakuvutia na Ac ndani?
Jiji lote limemezwa na bahari.. eh Mwenyezi Mungu tuhurumie.. najua dhambi zimezidi ndio maana watuadhibu!!
Wenye tamaa ya magari... thamani ya gari lako leo hii lingekuwa wapi kama hii ghalika ingetukumba Tanzania?? binadamu tumetelekeza magari yetu kuokoa uhai wetu....
tukiwa bize tunataka barabara za juu na chini na njia nne nne, badala ya kukesha kanisani na kumuomba Mungu.. leo hii wenzetu barabara hazina thamani tena... wanatamani wangejua saa au hata siku ya ghalika hii ili watubu zilizo Dhambi zao
Wanafunzi wakiwa wanatumia notes body kuangalia matokeo yao ya mitihani... wenzetu elo hii Japan Wanatumia notes body kupeana taarifa na kuona majina maybe ya wale waliosalimika au kunusurika
Eh mwenyezi Mungu naililia Japan, Tanzania na dunia yote maana hizi kwangu naamini ni ishara za kutuonyesha kwamba unachukizwa na madhambi tunayoyatenda kila kukicha.. niokoe roho yangu na wale wote wanaoamini kuna siku ya hukumu mbele yako siku moja....

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie