FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Saturday

TMH YAZINDUA KITUO CHA MICHEZO KWA AJILI YA WATOTO


Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos ambaye ni mgeni rasmii wa uzinduzi wa sherehe ya uzinduzi wa kituo hiki cha kuchezea watoto, akizungumza na wageni waalikwa...


Mwenyekiti wa kituo cha Tanzania Mitindo House,Khadija Mwanamboka akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla iliyofanyika leo mchana kigamboni katiza uzinduzi wa kituo cha michezo kwa watoto.Khadija amesema kuwa kituo hicho kimetengenezwa kwa msaada wa makampuni ya Bench Mark Productios,RBP OIL& Industrial Technology Ltd pamoja na Urban Pulse,ambacho kimegharimu shilingi za Kitanzania Milioni sita na laki saba.Udhamini wa ufunguzi wa kituo hicho umedhaminiwa na Kiondo Commonications International na Digital Art.Khadija aliongeza kuwa itahakikisha watoto Yatima wanapata fursa ya kucheza kama watoto wenye Wazazi na watajitahidi kuboresha kituo hicho kwa kuweka jukwaa la kuimba na kucheza pamoja na vifaa vya michezo ya watoto.

Hivi ndivyo watoto hawa walivyojiachia leo kuonesha furaha yao.....kwakuwa ufunguzi ulikuwa mchana..TMH walituandalia lunch baab kubwa ili kuweza kuweka matumbo sawa na kupata nguvu ya kucheza na watoto...


picha ya pamoja na watoto baada ya chakula....Moja kati ya ndoto kubwa za mwanamitindo wetu Fidelin Iranga ni kuasili mtoto na kuishi nae.. anaamini watoto wengi wasio na wazazi wanandoto nyingi za kutimiza hivyo kwake ni faraja kubwa kuona anamsaidi mtoto mmoja wapo


kila mtoto anahitaji upendo wa dhati bila kujali afya yake, rangi au jinsia... nimempenda huyu mtoto.. namuombea kwa
Mola apate baraka tele na afya njema ya kudumu...


Nilijaribu kupanda bembea hizi ili kujua uhodari na uwezo wake... zipo salama kabisa kwa watoto.. umecheck ilivyobeba mzigo hapo??
Baada ya shughuli nzima nilipata nafasi ya kupiga picha na the number one (Old is Gold Model) Fidelin Iranga( Tanzanian Lady Ga Ga )

4 comments:

 1. Anonymous12:44

  katika siku zote.. leo fide umejitahidi kujikoki na umependeza. yale ma make up yako machau umeyaacha.

  ReplyDelete
 2. Anonymous12:50

  nimegundua wewe dogo unamoyo wa upendo na huna majigambo kama hao mnaowaita mastaa huko bongo huku wadhiki kibao

  ReplyDelete
 3. dats08:34

  i just admire u 4 a brother as days go by,.. kip doing it. i love ur sense of style and ur simple lyf

  ReplyDelete
 4. Anonymous09:07

  Fide sipendi mi make up yako,nikikuonaga mpaka naota usiku,leo umetoka bomba usiwe unayapaka pls unantisha

  ReplyDelete

sema tukusikie