FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Tuesday

Flaviana Matata Azindua "FLAVIANA MATATA FOUNDATION"

Ikiwa ni siku chache tangu mafanikio ya binti mdogo wa kitanzania Flaviana matata kuonekana kutokana na kazi anayoifanya hivi sasa ya uanamitindo huko nchini marekani, Binti huyu ameamua kuzindua Foundation ambayo itakuwa ikijihusisha na uwezeshaji wa wanawake na watoto wasioweza kupata huduma mbali mbali za muhimu katika maisha yao.. Akizungumza wakati wa Uzinduzi huu Flaviana Matata amesema "Elimu ni jambo la muhimu kwa kila binadamu na linahitaji Fedha ili kuhakikisha linapatikana kwa wakati muafaka, hivyo nitajitahidi kupitia Flaviana Matata Foundation kuwawezesha wanawake na watoto kupata elimu bora!!
Mwanvita Makamba ambaye ni mmoja wa walezi wa Foundation hii akitoa neno la ufunguzi wakati wa uzinduzi wa Foundation hii uliofanyika ndani ya Hotel ya Kempisky!!
Wadau mbali mbali waliohudhuria uzinduzi huu kutoka kushoto Teddy mapunda, Babla Hassan And Salama jabir

More pictures za fashion na nyinginezo kutoka katika shughuli hii zinakuja.. hizi ni kwa msaada wa fullshangwe blog

Monday

Gaga "naichukia Video niliyofanya na Beyonce

Video ya Telephone ambayo aliifanya Lady gaga na Beyonce na kupata umaarufu mkubwa kwa mwaka jana imekuwa ikimkera sana lady Gaga..
Lady Gaga anasema,"siwezi hata kuitizama Video ile, naichukia kupita maelezo! mimi na Beyonce tuko Vizuri pamoja, lakini Video ile ina mambo mengi ya kipuuzi, nachokina kwa sasa ni ukosefu wa Idea za kutosha katika Video ile."

Katika video zake alizowahi kuzifanya lady Gaga anasema "Alejandro" ndio nyimbo anayoipenda video yake.. anasema anajua watu wengi wamekuwa hawaipendi video hii lakini yeye kwake ni kila kitu. alisema hayo alipokuwa akizungumza na Britain's Time Out magazine:

Weekend out


Weekend hii nilipata nafasi ya kuzunguka zunguka na one of my friend Neema, she wanted to do a small shopping and because i was free nikaamua kuzunguka nae mjini, mwisho wa safari zetu tukajikuta dukani kwa Amina designs!!
She is just a very sweet woman... was nice shopping at your stole Amina although sikupata chochote cha kiume zaidi ya lunch nzito na kuhaidiwa sneakers akirudi this month kutoka kuchukua new stock!!

Friday

Most Powerful Celebrities wa 2011

Nafasi ya kumi inasimamiwa na mcheza kikapu Lebron James, amejiingia kipato zaidi kupitia jezi yake kuuzika zaidi kwa mwaka huu na kiatu chake ndo kimeshika nafasi ya kwanza katika mauzo
9.Simon Cowell

8. Jon Bon Jovi, anamiliki bendi yenye miaka 28 katika tasnia ya burudani na haijawahi kulega lega, tour ya bendi yake kwa mwaka huu katika Chat ya Billboard ilitambulika kama tour iliyokuwa na faida zaidi ya mategemeo. bendi hii imewahi kutoa album iliyoingiza zaidi ya milioni 200 za kimarekani.


7.Taylor Swift bado anajitahidi kushangaa mafanikio yake kimuziki.. ambapo kwa mwaka janaa alijiingizia milioni 45 za kimarekaNi


6.Tiger wood,Tukiachana na skendo zilikuwa zikimuandama za mahusiano bado amebaki kuwa mchezaji wa golf mwenye kulipwa vizuri zaidi kuliko wote, kuonekana kwake katika uwanja wa mchezo huo anajiingizia milioni 3 na bado katika EA sport game amekuwa akifanya vizuri kwa takribani miaka 14.


5.Elton John,Anatambuliwa na kuheshimiwa na Malkia Elizabeth,ukiachana na charity events anazozifanya kwa mwaka mzima Sir Elton john kwa mwaka jana amefanya maonyesho 102 ambayo yamemuingizia kiasi kikubwa cha fedha,


4. Kundi la U2 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita wamejiingizia zaidi ya milioni 700 za kimarekani kwa kuuza ticket za maonyesho yao na kufanya show mbele ya mashabiki milion 7


3.Justin Bieber ukiachilia umri mdogo alionao, album yake ya My life 2.0 imefanya vizuri katika mauzo ya Filamu yake mpya ya Never say Never imemuingizia zaidi ya milioni 100 za kimarekani.


2. Oprah Winfrey,Ukiachana na kipindi chake cha television ambacho kwa hivi sasa kimefikia mwisho, mama huyu ameamua kuanzisha tv Cable inayoitwa OWN ambayo itaendelea kumuingizia kipato, katika account yake ana zaidi ya shilingi milioni 270 za kimarekani


Nafasi ya kwanza kasimama mwanadada Lady GaGA.. unaweza kumuita jila lolote hata The Next Lady Madona lakini haitaficha ukweli wa mafanikio aliyonayo kwa sasa, Amezalisha milioni 170 za kimarekani katika maonesho 137 kwa mwaka jana, ameuza zaidi ya album milioni 15, na ana mashabiki zaidi ya milioni 32 ndani ya facebook..


"Taarifa hizi ni kwa msaada wa Forbes"

Gomez na Justin Bieber watafuna raha Beach

Justin Bieber akiwa kijana mwenye umri wa miaka 17 tu ameanza kuenjoy maisha zaidi ya hata wale wenye umri mara mbili ya umri wake!! hivi karibuni kamera za mapaparazi ziliwabamba wakiponda raha katika pwani Maui.

We justin mbona taulo limekuzidi umri? na Selena naona una kitu cha mnyama mkononi!!Wednesday

Amber Amponda Kanye West.....

Weekend iliyopita wapenzi wawili ambao mapenzi yao kwa sasa yanashika Chat Wizzy Khalifa na Amber Rose walionekana wakipeana raha katikati ya club moja ya usiku jijini la Paris.

Tukiangalia kwa upande wa Amber Rose, katika cover story ya Gazeti la King, Amber alionekana kuponda mapenzi yake na Kanye West na kusema kwa wizzy ni kila kitu, nanukuu manenoo yake anasema,


"Kipindi nilipokuwa na Mpenzi wangu wa zamani (Kanye west) Sikuwa na Sauti kabisa kwake,Nilikuwa sielewi kila kitu, lakini kwa sasa napata kila kitu... Mimi na Wizy mapenzi yetu tumeweka wazi mbele ya dunia, hatufichi mambo yetu tunapendanaa na tunafurahia mapenzi yetu na tunataka watu wengine wfuate nyayo zetu katika mapenzi hakuna haja ya kuogopa kuwa katika mahusiano."Lil Wayne na Chombo Kipyaaaaa.

Mwanamziki mahiri wa Rap Lil Wayne jana alidakwa na mapaparazi akiponda raha na girlfriend wake mpya ndani ya Miami Beach, Mtandao mmoja maarufu wa mastaa wa mjini marekani umesema jamaa baada ya kufika ufukweni hapo alipata nafasi ya kupiga picha na mashabiki wake na kuendelea na shughuli zake za kupunga upepo ufukweni hapo.. mpaka wakati huu naandika habari hii sijapata jina la binti huyu mchanga.


As always it feels good to love and get loved, so tusishangae kupata rumors kwamba Bi dada anamimba ya mchizi


Tuesday

Best from Billboard Music Awards Red Carpet

Mary J
Keri Hilson

Kelly Rowland


Fergie


Michelle william
Monday

Them moment katika Red Carpet

April 22 style moto moto ilikamilisha round yake ya nne na ilikuwa ndo ya mwisho, Theme colour was Yellow na mimi nilijitupia hivi,
Full swagger za Jacque
Wadada walitupia yellow rose mkononi lilikuwa limebuniwa na Farha Sultan
As i always say...Sneakers ndo kiatu pekee kinanifanya kuwa confortable!!
Peace and love

Keyshia Cole afunga Ndoa na Boobie

Mwanamziki Keyshia Cole jana jioni amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Daniel "Boobie" Gibson baada ya kufunga ndoa yao hiyo walipata nafasi ya kuzunguka na helicopter ndani ya jiji la Las Vegas, baadae Boobie alitweet "Sasa imekamilika hakuna la zaidi ni Mr&Mrs Gibson, tunashukuru kwa kila dua njema mlizotuombea, leo ni usiku muhimu katika maisha yetu #sitaki maswali
Wawili hapa walivalishana pete ya uchumba january 20 na kutokana na matatizo ya hapa na pale ndoa yao ilikuwa ikipigwa kalenda mpaka siku ya jana walipokamilisha ndoto zao za kuwa mke na mume!!
Wawili hawa wamefanikiwa kupata Mtoto mmoja wa kiume aitwaye Daniel Jr.Thursday

Agushi kuvamiwa na majambazi ili kupata Ticket ya Oprah

Katika ticket zinazotafutwa kwa gharama yoyote ni ticket za final episodes za Oprah Winfrey Show.... katika tukio la kushangaza jamaaa mmoja anayefahamika kwa jina la Robert Spearing ajizushia kuvamiwa na majambazi na kupoteza ticket yake ya show ili aweze kupewa ticket nyingine jambo ambalo sikweli katika mtandao wa burudani nchini marekani ilipoandikwa habari hii wamesema jamaa alijipasua na jiwe usoni na kujikwangua mkononi ili kuonekana na majeraha ya kutosha kuwaweza kuconvice watu kumuelewa na kukubaliana nae kwamba alikumbwa na jambo hilo...

Katika mahojiano yake na police Robert amesema hakutaka mke wake amkasirikie kwa kukosa ticket hiyo ya show hivyo akaamua kufanya hayo aliyofanya ili kuweza kupata ticket za Oprah Winfrey finals....

Trina&Keyshia cole wachanganywa na BET Awards Nominees

Ikiwa ni siku chache tangu kutolewa kwa List ya wale wanaowania tuzo za BET kwa mwaka huu baadhi ya wasanii wamefunguka na kuonyesha hisia zao wazi kwa tuzo hizo kwa mwaka huu, ukiachilia wanamziki ambao wapo ndani ya kinyang'anyiro hicho na hisia zao wengine ambao hawakuwepo katika list hiyo wameonekana kuchanganyikiwa na kupitia kurasa zao katika social network wameamua kuandika what the feel about it...
Wakwanza alikuwa Keyshia Cole ambaye yeye aliandika..."Kwa miaka saba sasa nimekuwa katika game na nyimbo saba ambazo zimekuwa 1record lakini none of them got award and am still touring", akaongezea kwa kusema "It is what it is, this type of thing are the way they are. Am not upset about any of it in anyway. I hope everyone that goes has a wonderful time

Trina nae kupitia twitter ameandika...."Fuck BET" just short sentence can show how mad you are!! trina ameonekana kukasirishwa na kitendo cha wa master P kuwa katika tuzo hizi wakati yeye kashadondosha mixtape za kutosha sokoni na zinafanya vizuri alafu hayumo katika BET's Best Hip-Hop Artist

Beyonce Aiaga Oprah show kwa show kali....

Wiki ijayo ndo itakuwa mwisho wa Ile Reality show ya Oprah ambayo kwa kiasi kikubwa imebadilisha maisha ya Watu wengi ndani ya Marekani na dunia nzima kwa ujumla, katika kukamilisha baadhi ya vipindi vya mwisho kabisa vya show Hii mwana nyonga Beyonce aliakwa kufanya show ambapo kwa mara ya kwanza aliifanya live show ya nyimbo yake mpya ambayo inajulikana kwa jina la Run the World (Girls) it was the most exciting show kutokana na dance aliyofanya dada huyu na dancers wake
Beyonce, Oprah and one of fans during the show
Wednesday

This is creativity!! am inlove with this video-Maroon 5 - Misery

Mtoto wa Nje aliniachisha na Mke Wangu...Arnold Schwarzenegger

Mchezaji filamu maarufu duniani na aliyejizolea umaarufu mwingi miaka ya 90 Arnold Schwarzenegger amefunguka na kusema kuwa Mke wake alimuacha kutokana na maumivu aliyoyapataa baada ya kugundua mchizi amemtundika mimba mmoja wa wafanyakazi wake. inasemekana miaka 10 iliyopita jamaa ndo alifanya hiyo kitu.... nukuu katika mtandao zinasema...

Arnold is Confessing that the reason his wife left him its its because he got a memberof their household staff pregnant 10 years ago

Tuesday

Many thanx to Shamim Mwasha-this is my new Perfume

Tar 23/3 ya kila mwaka huwa naazimisha siku yangu za kuzaliwa na mwaka huu nilifanya the same thing na picha niliweka hapa katika blog kwa miakamitatu iliyopita nilikuwa natumia Perfume inatwa Dunhil Desire na mwaka jana nilijaribu kutumia perfume za Antonia Benderaz... ila sasa nahisi nahamia kwa Channel kutokana na msukumo kutoka kwa fashion Star wetu wa bongo Shamim Mwasha

Katika birthday yangu ya mwaka huu Shamim kaniletee allure Home Sport kama zawadi kwangu.. nilipoigusa tu nilihisi nimeipenda kabla hata sijajinyunyiza mwilini lakini leo naadmit katika perfume zote nilizowahi kutumia hii inanifanya najisikia huru kichizi nikijipulizia!! kwakuwa nachukia harufu ya jasho la mtu naamini nikiombwa zawadi na mtu nitampelekea perfume kwanza na mengine yatafuata!! so Versace, DnG mmenikosa for now!! mimi na Allure!! by the way ni 79$ na kwa duty free unaipata kwa 69$!! so ndugu zangu mkiitaji bei hiyo hapo mmtafute shamim mwasha kupitia www.8020fashions.blogspot.com

Monday

Kanye West Ajianika na Totoz France

Rapper maarufu Duniani Kanye West jana alionekana kupitia balcony ya chumba chake ndani ya hotel ya Carlton in Cannes France, Mr. West is in France for the Cannes Film Festival however he decided to take some time out of his busy schedule to put on a kissing show for the paparazzi.hizi chini ni baadhi ya picha zaidi zilizopatikana kutoka katika hili tukio la mwaka!!