FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Friday

Most Powerful Celebrities wa 2011

Nafasi ya kumi inasimamiwa na mcheza kikapu Lebron James, amejiingia kipato zaidi kupitia jezi yake kuuzika zaidi kwa mwaka huu na kiatu chake ndo kimeshika nafasi ya kwanza katika mauzo
9.Simon Cowell

8. Jon Bon Jovi, anamiliki bendi yenye miaka 28 katika tasnia ya burudani na haijawahi kulega lega, tour ya bendi yake kwa mwaka huu katika Chat ya Billboard ilitambulika kama tour iliyokuwa na faida zaidi ya mategemeo. bendi hii imewahi kutoa album iliyoingiza zaidi ya milioni 200 za kimarekani.


7.Taylor Swift bado anajitahidi kushangaa mafanikio yake kimuziki.. ambapo kwa mwaka janaa alijiingizia milioni 45 za kimarekaNi


6.Tiger wood,Tukiachana na skendo zilikuwa zikimuandama za mahusiano bado amebaki kuwa mchezaji wa golf mwenye kulipwa vizuri zaidi kuliko wote, kuonekana kwake katika uwanja wa mchezo huo anajiingizia milioni 3 na bado katika EA sport game amekuwa akifanya vizuri kwa takribani miaka 14.


5.Elton John,Anatambuliwa na kuheshimiwa na Malkia Elizabeth,ukiachana na charity events anazozifanya kwa mwaka mzima Sir Elton john kwa mwaka jana amefanya maonyesho 102 ambayo yamemuingizia kiasi kikubwa cha fedha,


4. Kundi la U2 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita wamejiingizia zaidi ya milioni 700 za kimarekani kwa kuuza ticket za maonyesho yao na kufanya show mbele ya mashabiki milion 7


3.Justin Bieber ukiachilia umri mdogo alionao, album yake ya My life 2.0 imefanya vizuri katika mauzo ya Filamu yake mpya ya Never say Never imemuingizia zaidi ya milioni 100 za kimarekani.


2. Oprah Winfrey,Ukiachana na kipindi chake cha television ambacho kwa hivi sasa kimefikia mwisho, mama huyu ameamua kuanzisha tv Cable inayoitwa OWN ambayo itaendelea kumuingizia kipato, katika account yake ana zaidi ya shilingi milioni 270 za kimarekani


Nafasi ya kwanza kasimama mwanadada Lady GaGA.. unaweza kumuita jila lolote hata The Next Lady Madona lakini haitaficha ukweli wa mafanikio aliyonayo kwa sasa, Amezalisha milioni 170 za kimarekani katika maonesho 137 kwa mwaka jana, ameuza zaidi ya album milioni 15, na ana mashabiki zaidi ya milioni 32 ndani ya facebook..


"Taarifa hizi ni kwa msaada wa Forbes"

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie