FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Wednesday

Vijana wa Kitanzania Wenye sauti zaidi Bongo!!


Akiwa ni mtangazaji mwenye kipato zaidi kupitia kazi yake ya utangazaji, mume wa mwanamziki tajiri zaidi,meneja wa bendi maarufu tanzania.. amejaliwa sauti ya kugusa umma wa watanzania. manneo yake machache anayotamka yanaweza kubadilisha maisha yako kwa muda mfupi.. wasikilizaji wa jahazi watakuwa wanakubaliana na mimi.

Working as head of TBC international.. taji liundi amekuwa na sauti ya kuvutia na kugusa watu wa rika mbali mbali hadi kuweza kuaminika na raisi wa Tanzania. Taji liundi ni mmoja wa washereheshaji wa kutegemewa na nchi kuanzia shughuli ndogo ndogo mapka za ikulu!! hii ni kutokana na great personality aliyonayo
!!

Ni wasichana wachache sana wanaojaliwa uzuri na vipaji lukuki.. akijulikana kwa jina la Jokate.. amefanikiwa kufikia nafasi za juu katika mashindano ya urembo na baada ya hapo kujikita katika mitindo na uigizaji.. lakini mafanikio yake yameonekana zaidi katika swala la matumizi ya sauti kuwa mshereheshaji na muingizaji sauti katika matangazo mbali mbali ya redio au Tv tanzania.. anakubalika sana kwa wapenzi wa mitindo tanzania na wasichana wengi wamejikita katika mitindo kutokana na kuvutiwa nae!!

Hot and sexy salama Jabir.. ameweza kubadilisha vijana wengi wanaofanya muziki wa bongo flava.. mwanzoni watu wengi hawakumuelewa lakini mabadiliko ya ubora wa muziki pamoja na video zao unaleta taswira mpya katika muziki wa kitanzania.. inaaminika kuwa nyimbo yako salama akiipitisha inapita na kukubalika tanzania nzima!

Malkia wa sauti Tanzania Lady jay Dee.. kupitia mashairi matamu ya nyimbo zake amefanikiwa kukubalika sana na kupendwa na Watanzania wa rika zote bila kujali kipato chao au maisha yao.. hii ni kutokana na nyimbo zake nyingi kuwatoa machozi baadhi ya mabinti kutokana na mashairi yenye ujumbe mzito hasa katika swala zima la mapenzi.. Yeye ni balozi wa maralia kupitia kampeni ya Zinduka na balozi wa CCBRT kupitia kampeni ya kuondoa Fistula tanzania!!

B12, Hamis Mandi na kwa sasa anajulikana zaidi kwa jina la Navigator!! kupitia sanaa au tasnia ya utangazaji. B12 amewezaa kuwateka vijana wengi wa kitanzania na sauti yake kupata umaarufu zaidi unapokuja katika swala la jingle kwa ajili ya matamasha mbali mbali hasa yanayohusu vijana!! ni mmoja kati ya watangazaji wenye kuweza kupewa jukumu la kuwa Balozi wa Kampeni yoyoye na ikafanikiwa kwaa kiasi kikubwa!!


Akiwa ni mama wa watoto wawili na mke aliyehamishia makazi yake nje ya tanzania! Mange Kimambi tanzanian fashionista ameweza kupata mashabiki wengi zaidi kupitia blog yake hii inamaanisha kuwa mambo mengi anayoweka katika blog yake yanawagusa wengi katika maisha yao kila siku!! namuita mpambanaji asiyechoka kutafuta lile linalompa furaha katika maisha yake! Diva mange !!

Kwa muda mfupi alikuwa mbunge wa viti maalumu Halima mdee ameweza kupambana katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo la kawe na kufanikiwa kulitwaa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema.. uwezo aliojaliwa na mwenyezi Mungu ndo umemuwezesha kulitwaa jimbo la kawe kwa kasi kubwa!!

King wa Bongo crunk!! Anatambulika kwa jina la Cpwaa.. ukizungumzia vijana wakitanzania wanaogusa wengi kupitia mziki wa bongo flava, Cpwaa anashika nafasi ya juu zaidi.. hii ni kutokana na personality aliyonayo!!


Nikiwa mmoja kati yao.. nimejaliwa vipaji kadhaa, nikiwa mmoja wa trainers wa models mwenye kulipwa vizuri, model wa kwanza tanzania kufanya kazi na Naomi Campbell alipokuwa tanzania, msimamizi wa Modelling event wa kutegemewa na niliye katika mchakato wa kuwa Balozi wa kituo cha watoto yatima hivi karibuni..Mwenyezi Mungu niwezeshe nitimize malengo yangu!!

Ikumbuke ni jinsi aonavyo mmiliki wa Mvutokwanza blog

5 comments:

 1. Anonymous11:28

  Hahahahahaha "mwanamuziki tajiri Tanzania".How do u define tajiri?!

  ReplyDelete
 2. Kweli mvuto kwanza, sikumbuki kufiaka hapa, nakiri umevutia kwa vitu vyako hongera

  ReplyDelete
 3. tajiri? binadamu anaweza kuendesha maisha yake bila kutegeme mtu mwingine, mwenye kipato kizuri kifedha.. ninauhakika kuhusu swala la kipato.. mwenye roho ya kusaidia wale wenye shida na kukwama kimaisha. hili nalo kama unahitaji ushaidi naweza kukupa!!

  ReplyDelete
 4. Anonymous07:04

  Hayo yote mengineyo nilikuwa nauliza maana ya neno tajiri basi,makubwa haya ha ha ha ha ha.Mwanamuziki tajiri ha ha ha ha ha.Huwa unanifurahisha sana sababu unajua kupamba mtu.Ila cha msingi ni kwamba Jaydee si tajiri bali ana uwezo na mafanikio naomba uelewe hilo.Tanzania hakuna tajiri kuna wenye uwezo wa kifedha na kujiweza labda utajiri wa roho.Si kwamba simpendi Jaydee I've been a big fun of Jaydee since album yao ya asubuhi njema.Ila sidhani hata kama yeye atatpita hapa atakubaliana na wewe unayoyasema kwamba ni tajiri.

  ReplyDelete
 5. like the blog.im a fellow east african blogger. check out my blog n follow if you like.http://justcozisayso.blogspot.com/ mbabaziannet.blogspot.com

  ReplyDelete

sema tukusikie