FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Saturday

STEVEN KANUMBA AFARIKI KATIKA HALI YA UTATA: LULU MICHAEL ABEBESHWA LAWAMA ZOTE


JOHARI AKIHOJIWA

NADHANI NIANZE NA PICHA ZA MATUKIO AMBAZO  NIMEZIPATA KUPITIA 8020FASHIONS ZA HALI ILIVYOKUWA KABLA  WATU HAWAJAA ASUBUHI HII. HUYU PICHANI JUU NI MSANII JACKLINE WOLPER ALIYEZIMIA BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO... 

MDOGO WA MAREHEMU NINAYEMFAHAMU KWA JINA LA SETH.... NAMWONEA HURUMA MAANA HAJAPATA MUDA WA KUPUMZIKA KUTOKA SAA SABA USIKU HILI TUKIO LILIPOTOKEA.....

UMATI WA WATANZANIA ULIKUSANYIKA HAPA NYUMBANI  KWAKE SINZA VATCAN

MSANII WEMA SEPETU ALIKUWA MMOJA KATI YA WATU WA KWANZA KABISA KUFIKA ENEO LA TUKIO.... 

HAYA SASA HABARI NILIZONAZO NI KWAMBA.... KWA KIPINDI KIREFU LULU MICHAEL NA STEVEN KANUMBA WAMEKUWA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWA SIRI...  NA JANA USIKU LULU MICHAEL ALIENDA NYUMBANI KWA KANUMBA KAMA WALIVYO WAPENZI WOTE BAADA YA KUFIKA ALIMKUTA KANUMBA NA MDOGO WAKE WAKIWA SITTING ROOM, BAADA YA LULU KUINGIA KULITOKEA MKWARUZANO MDOGO KATI YA KANUMBA NA LULU NA WAKAAMUA KUINGIA NDANI ILI KUYAZUNGUMZA MAMBO YAO KWANI YALIONEKANA KUWA NIYANAYOWAHUSU WAO WAWILI... MUDA MFUPI BAADA YA KUINGIA NDANI ULE MKWARUZANO ULIZIDI KUWA MKUBWA KULINGANA NA UPAZAJI WA SAUTI ZA WAWILI HAO... MDOGO WA KANUMBA ANASEMA BAADAE KIDOGO NI KAMA SAUTI ZILIKATIKA NA LULU AKATOKA NJE NA KUMWITA AINGIE CHUMBANI, ALIPOINGIA CHUMBANI ALIMKUTA KANUMBA AKIWA AMEANGUKA CHINI NA HANA FAHAMU, SETH KWA HARAKA ALITOKA NJE NA KUKIMBIA KWENDA KUTAFUTA DAKTARI, ALIPORUDI NYUMBANI ALISHANGAA KUMKUTA MAREHEMU PEKE YAKE NA LULU HAONEKANI.... HIYO NDIO HALI HALISI.. KILICHOTOKEA NDANI NI LULU PEKEE ANAYEWEZA KUELEZA NINI KIMPELEKEA KANUMBA KUIAGA DUNIA... KWA HIVI SASA LULU MICHAEL YUPO OSTERBAY POLICE KWA UCHUNGUZI ZAIDI.....
MAZISHI YATAFANYIKA JUMANNE IJAYO ILA MPAKA SASA HAIJAJULIKANA KAMA ATAZIKWA HAPA JIJINI DAR ES SALAAM AU KWAO BUKOBA...

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie