FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Friday

Mvutokwanza inapenda kuwapa Pole watanzania Wote walioathirika na Mabomu ya Gongolamboto

Nyumba ni zetu wenyewe, magari ni ya kwetu wenyewe na hata mali ni za kwetu wenyewe lakini ilifika wkati hatukuona umuhimu wake zaidi ya kuokoa maisha yetu....Hili ni fundisho kwa kila binadamu..siku ya kifo hakuna anayejua wala saa na sekunde... tumuombe Mungu msamaha kwa yale yote maovu tuyatendayo.. wapo ambao leo hawapo duniani kutokana na milipuko ya juzi na ipo siku mimi sitakuwepo au wewe utakuwepo.. je tupo tayari kwa huko tuendako baada ya haya maisha haya?? nimekuwa nikitokwa na machozi nitazamapo picha hizi.. najiuliza je na mimi ningekuwa mmoja ya waliofariki? ni msafi wa kurudi kwa Muumba? tubadili mienendo na tabia zetu na kuachana na kelele kwa rais au serikali.. angalia maisha yako na upendo wako kwa kila anaekuzunguka? ni watu wangapi leo hii umegombana nao na hutaki hata kuwasikia? unajiona wewe ni Mungu kuchagua anayekufaa na asiyekufaa?
Ardhi yetu nzuri na yenye rutuba ilibadilika kuwa kiwanja cha kutua makombora ya kijeshi.. simlaumu Raisi, kamanda mkuu au mkuu wa majeshi kwakuwa kila jambo linatokea hapa duniani Mwenyezi Mungu alishalijua kabla na akaliacha litokee. tuepushe marumbano na kuwasaidia walio katika kipindi kigumu kwa sasa kwa kukosa mavazi, malazi na chakula.. na tutapata thawabu kwa mungu badala ya kupiga kelele zisizo na na faida kwa waathirika wa janga hili
Tupo garini lakini hata hatujui tuendako... ni katika kunusuru roho zetu zilizojawa na hofu.....
Sikuwahi kutegemea ipo siku tutakuwa kama wakimbizi!! Eh Mungu ibariki Nchi yetu na kuiepusha na mabalaa yote!!
Jukumu la kuokoa watoto kwa wakati huu halikujali baba wala mama kila mmoja kwa uwezo wake alijitahidi kuhakikisha watoto wetu wako salama ingawa wapo waliopotea kabisaa kwa mshtuko....
tukiachana na hayo hapo juu hivi kunatatizo gani tukipewa taarifa juu ya idadi sahihi ya waliofariki? Arjezeera inatangaza idadi yake, CNN idadi yake na vyombo vya nchi yetu idadi yake!1 tumwamini nani sasa???????

No comments:

Post a Comment

sema tukusikie