
Sikuhizi Sharobaro sharti nguo ya ndani ionekani akivaa mlegezo, enzi hizo masharobaro walikuwepo lakini walikuwa wanapiga shati la uji uji na juu "nibanie chini niachie"

Kiduku kilikuwepo enzi hizo lakini sharti uinamie mbele sio nyuma ili kulinda ushalama wako, sikuhizi tunainamia mbele, we mtoto nyuma nani anakulinda?

Nyie mnaenda Beach za Mzungu, enzi hizo picnik ni mtoni, mamba na kenge tunaogelea nao tu

Mnaenda photopoint sikuhizi na vibag vya LV au Gucci, enzi hizo unabeba kahawa yako na unapozi nayo katika picha kama una mimina hivi

Kiduku sharti upanue miguu ili kuweza kuruhusu mzunguko wa hewa safi na chafu wakati wa uchezaji

sikuhizi mnabeach wear, enzi hizo ni chochote we unavaa ukitaka kwenda kuogelea
No comments:
Post a Comment
sema tukusikie