
Ufukweni au beach kama wengi mlivyozoea mara nyingi ni eneo ambalo huwa tunaenda kupunga upepo na kutuliza akili zetu kutokana na yale tuliyopitia kwa kipindi kilichopita! familia nyingi au vijana wengi kama nijuavyo mimi hupenda kwenda ufukweni wakati wa weekend hii ni kutokana na kuwa ndio wakati pekee tunapata nasi.
Tukumbushane mambo ya muhimu uendapo ufukweni ili usiwe tofauti na wenzio utakaokutana nao huko, kwa vijana wakiume hizi ndizo kaptula zinazotufaa kwakuwa hazibaki na maji mwili wala kushika maungo yetu maana kuna watu huwa hawana amani kuogelea na nguo zao za ndani kwakuwa huwa wanahisi wanajichora maungo yao, hivyo basi ukipata kaptula kama hizi mambo yako yatakuwa salama kabisa.








Kabla ya kutumia lotion hizi jitahidi kumuona mtaalamu wa ngozi ili uweze kupata lotion inayoendana na ngozi yako maana lotion nyingi za jua zimetengenezwa kwa ngozi za watu weupe (wazungu)
No comments:
Post a Comment
sema tukusikie