FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Monday

Tanga Yasimama Wima na Burudani ya Serengeti Fiesta

This weekend nilikuwa Tanga katika Fiesta, naonekana kwa mbali katika picha hiyo hapo juu nikiwa na Antu na Pako mmoja wa madancer mahiri Bongo,Kwakweli i had a very good time katika mji huu maana ndio ilikuwa mara ya kwanza kutia kambi Tanga, kuna mengi niliyofaidi ila kwa upande wa burudani on stage, hawa ndio walionipagawisha!!
Shetta ni mmoja wa wasanii ambao kwangu nilikuwa nawaona ni wakawaida sana ila daah show aliyoifanya Tanga napenda kusema yeye ni mmoja wa wasanii wazuri juu ya jukwaa, napenda show ya kucheza aliyofungua nayo kabla hajaanza kuimba!! Shetta Your the Best.

Mwana FA utabaki kuwa kaka yao katika muziki, one man on stage na bado unaenjoy with no complains?? alifunika mbaya na ile ngoma ya Unanijua au unanisikia??

Linex wa Mama Halima he was the BEst kwa upande wangu, watu walikuwa wamepoooa lakini aliwaamsha kwa shangwe za ajabu nahisi ni kutokana na muziki wake kupendwa sana ndani ya Tanga.

Katika watu ambao hawajali wewe utasema nini as long he is doing what he loves the most ni Bob Junior, alipiga show ya nguvu na upande wa mavazi alinikosha sana, Respect kwako Bob Junior

For me, He is a king of soul, muziki wake unagusa hisia za ndani kabisa kwa yule mpenda burudani ya muziki, Ben Paul alinirusha vya kutosha na new track yake inayojulikana kama Number one fan.

After all those shows nje ya Tanzania unategemea nini Tena kutoka kwake?? mwite mkali wa Stage Ally Kiba mzee wa Dushele, tulidusheleka kweli kweli tanga.

1 comment:

  1. Anonymous04:25

    poleeeeeeeeni na pili hongereni sana hata hku mzee
    wa dushelele yupo up miaka 100 ITS MOHD MAUKWE

    ReplyDelete

sema tukusikie