FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Thursday

Michelle Obama

What makes her so powerful? kuna mambo mengi ambayo yanasababisha mwanamke yoyote kuwa na nguvu duniani pindi anapopewa nafasi ya kutumikia Jamii au eneo fulani lenye watu wa tabaka fulaniKatika List ya forbes iliyotoka mwaka jana wa 2010 Michelle Obama mke wa Rais wa marekani Barack Obama alitajwa kuwa kati ya Wanawake wenye nguvu zaidi, hii nguvu nayoongelewa hapa si nguvu ya kupambana vita au kupindua nchi ila ni nguvu ya kuweza kusimama mbele ya jamii na kusikilizwa pamoja na kugusa hisia za watu wengi wanakusikiliza kwa wakati huo.Toka kuanza kutumikia taifa lenye nguvu dunia Marekani Michelle amejitahidi kuishi maisha yake kama wanawake wengine hii inamaanisha kuwa amekuwa mshauri mzuri kwa mumewe, kuwa mama mwenye kujali mabinti zake wawili, ana mbwa pia ambaye amekuwa anamjali, hajajisahau yeye binafsi kimuonekano kitu ambacho kimemfanya kuwa fashion Icon, unadhani ni shughuli ndogo kuweza kufanya hayo yote ukiwa ni mke wa Raisi? hii yote inatoka na kuwa na wasaidizi wenye kuzijua kazi zao na kuhakikisha hawamwagushi, ukijiona una wadhifa mkubwa popote pale either wewe ni msanii wa muziki, muigizaji, mkurugenzi au mbunge tafuta watu wa kukusaidia kusimamia muonekano wako mbele ya jamii, you need stylist, you need meneja mahusiano(PR) na hata mwandishi wako binafsi ili kuweza kusimamia muonekano wako kwa jamii.Wakina mama Wengi ambao waume zao wamejaliwa nyazifa wameshindwa kuwa na muda kwa familia zao na muda mwingi kuwa katika majukwaa ya siasa na busy na shughuli mbalimbali za starehe namaanisha hauwakosi katika hafla mbalimbali za starehe!! watoto wenu mnawaacha wapi?Being a wife of the most powerful man turned you to be powerful woman hivyo basi tumieni nyazifa mnazozipata kuitumikia familia yako na jamii yako inayokuangalia kwa kipindi hicho! much respect Michelle Obama

1 comment:

  1. Anonymous05:51

    KAKA UKO RIGHT KABISA YAANI ULIYASEMA HILO JEMBE LA OBAMA.NICE GUY MARRIED TO A PERFECT WIFE.

    ReplyDelete

sema tukusikie